Friday, December 18, 2015

YA MAJABVI wa simba yamefika pabaya...UONGOZI, LOLOTE NA LIWE.



Uongozi wa klabu ya Simba umesema kiungo wao wa kimataifa wa Zimbabwe Justice Majabvi kama anataka kuondoka kwenye klabu hiyo ni ruksa kufanya hivyo kutokana na mgogoro uliopo kati ya
uongozi na nyota huyo wa nafasi ya ukabaji kwenye kikosi cha ‘wekundu wa Msimbazi’
                                      Kiungo wa Simba SC Justice Majabvi
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC Zacharia Hans Poppe amesema hata kama kuna vitu hawajatimiza kwa mchezaji huyo, hatakiwi kwenda kuzungumza nje ya klabu kwasababu mkataba wake unamzuia yeye kwenda kuzungumza
nje na kama anafikiri atasaidiwa na vyombo vya habari basi aende akadai hakai yake huko.
“Aende zake tu kwani tunatabu gani sisi. Kama kuna vitu tumetimiza au hatujatimiza hatakiwi kwenda kuanza kupayuka maneno hadharani
na mkataba unamnyima yeye nafasi ya kwenda kuzungumza na vyombo vya hari, yeye kama anafikiri atasaidiwa na vyombo vya habari basi aende akadai huko”, amesema Hans Poppe boss wa usajili wa klabu ya Simba.

No comments:

Post a Comment




Label 14

Label 14

Swimming

Label 15

Label 3

Label 4